Unknown Unknown Author
Title: Simba na Yanga zaamuriwa kumaliza tatizo la Kessy
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mnweyekiti wa hadhi na Sheria za wachezaji amesema soka si mchezo wa uhasama na kukomoana hivyo Simba na Yanga zikae mezani kumaliza tofa...
Mnweyekiti wa hadhi na Sheria za wachezaji amesema soka si mchezo wa uhasama na kukomoana hivyo Simba na Yanga zikae mezani kumaliza tofauti hizo
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji imezitaka klabu za Simba na Yanga kukaa chini na kumalizana  suala la usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Richard Sinamtwa, ameiambia Goal, ametoa nafasi hiyo ili kuondoa uhasama pande zote mbili lakini endapo watashindwa kuafikiana kwa siku tatu ambazo wamezitoa swala hilo litarudi mezani kwake nay eye atalitolea maamuzi kwa kufuata kanuni na sheria zinazoongoza soka la Tanzania.
“Ningependa viongozi wa klabu hizi mbili za Simba na Yanga kukutana na kulimaliza tatizo hili kirafiki kabisa kwa sababu soka sio kukomoana ni furaha na ajira pia lakini wakishindwa itabidi Kamati ifanye kazi yake kwa kutumia kanuni na Sheria zilizopo ili kulipatia ufumbuzi swala hilo,” amesema Sinamtwa.
Klabu ya Simba imewasilisha baua mbili kwenye Kamati hiyo ikiilalamikia mchezaji huyo kuhalalishwa kuitumikia Yanga wakati usajili wake ulifanywa kimakosa hali yakuwa ana mkataba wa kuitumikia Simba na nyingine ni Kessy kuanza kufanya kazi na Yanga huku akiwa na mkataba na Simba.
Tayari Kamati hiyo ilimruhusu Kessy, kuendelea kuichezea Yanga kwenye mechi za ligi ya Vodacom, kwa sababu kesi iliyowasilishwa mezani haikuwa na matatizo kwenye usajili wake bali ilikuwa ni ya madai jambo ambalo kamati iliamua kumruhusu kucheza ili asije kupoteza kiwango chake huku madai hayo yakiendelea.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top