toniking toniking Author
Title: Kibaha wamkataa DED mbele ya RC
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
                MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jeniffer Omolo amepata wakati mgumu baada ya wafanyabiashara kumkataa na ku...

                MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jeniffer Omolo amepata wakati mgumu baada ya wafanyabiashara kumkataa na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo aondoke naye wakidai ameshindwa kuwajengea soko.
Kutokana na malalamiko ya wafanyabiashara hao, Mkuu wa Mkoa alitoa siku 90 sawa na miezi mitatu kwa mkurugenzi na watumishi wengine kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa soko na stendi ya daladala.
Hayo yalitokea wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Bwawani, Kibaha Maili Moja ukihusisha waathirika wa bomoabomoa wa Maili Moja wakiwemo wafanyabiashara wa soko la mkoa la Maili Moja.
Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jafari Mkomwele, alisimama na kumweleza Mkuu wa Mkoa kuwa, Mkurugenzi huyo aliwaahidi wafanyabiashara kuwa fedha za kujenga soko zipo tangu mwaka 2014, lakini hadi leo halijajengwa.
“Sisi tunaona kuwa hii ni siasa ni bora ukaondoka naye kwani tunaona hatujatendewa haki ni bora tuanze kujenga mji mpya na mkurugenzi mpya na siyo huyu. Alituzindulia mchoro wa soko tangu mwaka 2014 tunaona ni vyema ukaondoka naye,” alisema Mkomwele.
Alisema mji wa Kibaha unashindwa kuendelea kutokana na watendaji wa Halmashauri kushindwa kuwajibika na kuwafanya watu wachoke kwa kufanya kazi wakiwa ofisini bila kujua changamoto za watu. Akijibu kwa niaba ya Mkurugenzi, Ndikilo alisema changamoto ya fedha ndiyo imesababisha ujenzi wa soko na kwamba tatizo si mkurugenzi.
Ndikilo alisema mkurugenzi huyo alirudishwa Kibaha baada ya kuonekana kuwa halmashauri yake ni moja ya halmashauri zinazokusanya mapato makubwa nchini.
“Mkurugenzi wetu ni mchapakazi mzuri kwani Halmashauri yake mbali ya kuwa moja ya halmashauri zinazokusanya mapato vizuri pia ina hati safi,” alisema Ndikilo.
Aidha, alisema zikiisha siku 90 ataitisha mkutano mbele ya wananchi ambao watapiga kura endapo kutakuwa na mtendaji ambaye ni kero atapigiwa kura na yeye ataondoka naye, kwani serikali ya sasa si ya kubembelezana.
Kufuatia hali hiyo aliwataka watendaji kufanya kazi na kama atakuwepo mtumishi asiyewajibika na akitajwa na wananchi ataondoka naye na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi, kwani masuala yao yatakwenda sawa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top