toniking toniking Author
Title: UWEZO WA NGISI KUJIBADILI RANGI
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
  UWEZO WA NGISI KUJIBADILI RANGI Ngisi  anayeitwa cuttlefish anauwezo wa kujibadili rangi na ujificha hili asiweze  kuonwa na maa...

 UWEZO WA NGISI KUJIBADILI RANGI



Ngisi anayeitwa cuttlefish anauwezo wa kujibadili rangi na ujificha hili asiweze  kuonwa na maadui zake,pia asiweze kuonekana na mwanadamu .Kulingana na ripoti moja ,Ngisi hao "wanafahamika kuwa na rangi mbali mbali na wanaweza kubadili rangi kwa njia ya kustahajabisha".


Ngisi huyo ujibadili rangi kwa kutumia chembe chembe fulani ndogo za pekee zilizo chini ya ngozi yake.Chembe hizo huwa na vifuko vilivyo jaa rangi mbalimbali vilivyo zungukwa na misuli midogo sana.
Ngisi uyo anapo taka kujibadili rangi ili ajifiche,Ubongo wake utuma tahalifa ya kukaza misuli ilio zunguka vifuko ivyo,kisha vifuko ivyo na misuli utanuka na rangi ya ngisi ubadilika mara moja.Mbali na kutumia uwezo uwo kwa kujificha ,Pia utumia uwezo huo kuvutia ngisi wengine na ata kuwasiliana nao.


Wataalamu katika chuo kikuu cha Bristol Ungereza Walitengeneza ngozi  kama ya Ngisi huyo,Waliweka visahani vya mpira mweusi katika vitundu vidogo vinavyo fanya kama misuli ya ngisi uyo ,Watafiti hao walipo unganisha umeme katika ngozi iyo,Misuli iyo ilitanuka na kubadili rangi ya ngozi iyo.
Utafiti ulio fanya kuusu ngozi ya Ngisi uyo unaweza kutumia kutengeneza nguo ambazo uweza kubadili rangi,
JONATHAN ROSSISTER alifafanua misuli iyo uwa " lain na imebuniwa kwa ustadi wa hali ya juu",
Na kusema ipo siku moja watu watavaa nguo zilizo buniwa na kutengenezwa kwa kutegemea muundo wa ngozi ya Ngisi uyo "CUTTLEFISH" zinazo weza kubadili rangi ,iwe kwa kujificha au mtindo.
(video)


                                               


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top