Kama anaichezea timu yako, unampenda, kama anacheza dhidi ya timu yako unahisi kama unataka kushika mkia wake na kumwambia wewe ni..... unajua nini utakachosema mwenyewe.
Kwa sasa, mashabiki wa Manchester United wanamuona kama Cantona mpya; Mungu wa soka anayeweza kuirejesha hadhi ya Old Trafford.
Hilo linaweza kutimia kwa sababu popote anapokuwa Mswedeni huyo, huwa anashinda na mkali wa kucheka na nyavu.
Anacheza kwa swaga - hakuna tatizo katika hili - na mwenye kasi isiyo na mpinzani. Hakuna ubishi kwamba mkali huyu ana kipaji cha kipekee.
Ibra ana sifa tele na amethibitisha hilo katika hatua kibao tofauti na Ligi ya Mabingwa Ulaya, inafahamika.
Ubora wake na kujiamini vinafahamika na wachezaji wote wanaokuwa naye dimbani. United tayari wanampenda sana.
Akiongea na Geoff Shreeves katika mahojiano na kituo cha Sky Sports, alisema: "Mimi si mtu wa fujo, ni mtu wa kawaida.
"Watu wanaitafsiri vibaya taswira yangu kwamba mimi ni kijana mbaya, lakini mimi ni mtu wa familia ninayejali familia yangu. Lakini ninapotia mguu wangu dimbani nakuwa simba.
"Sidhani kama mimi ni mkatili kama wanavyodhani wengi. Najiamini na nauamini uwezo wangu. Huo si ukatili."