Unknown Unknown Author
Title: Van der Pluim: Samatta ni mfano wa kuigwa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kiwango kinachoonyeshwa na mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Samatta, kimemgusa Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm na m...
Kiwango kinachoonyeshwa na mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Samatta, kimemgusa Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm na mwisho akafafanua kuhusiana na uwezekano wa siku moja staa huyo kucheza katika timu za Ligi Kuu Uingereza.
Nahodha huyo wa Taifa Stars, amekuwa msaada mkubwa kwa sasa katika timu hiyo ya Genk na kufanikiwa kufunga mabao manne katika mechi nne alizoichezea timu hiyo kwenye msimu mpya wa 2016/17 na kuwa kileleni mwa msimamo wa wafungaji bora wa ligi hiyo mpaka sasa.
Pia juzi Alhamisi Samatta aliiongoza Genk kutinga kwenye michuano ya Europa League.
Kocha huyo wa Yanga ameeleza kwamba Samatta ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengi wa Tanzania, si kwa uchezaji tu bali hata nidhamu na tabia yake uwanjani na vingine vingi ambavyo vimempa mafanikio na kufikia hapo alipo.
Kupitia gazeti la Championi kocha huyo wa Yanga ameainisha ubora wa nyota huyo wa Genk na kuelezea zaidi kuwa wachezaji wa Tanzania wanao mfano wa kuiga hadi sasa.
“Samatta ana kasi, ubora, akili, tabia njema na ni mfano mzuri kabisa wa kuigwa na wachezaji wengi wa Tanzania kama wanahitaji kufika alipofika Samatta, bado nayaona mengi mazuri yapo mbele yake kutokana na heshima ya mpira aliyonayo.
“Nimesikia pia akihusishwa kuweza kuishawishi Manchester United siku

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top