Unknown Unknown Author
Title: wachezaji wa bara wanaotakiwa kulinda nafasi zao xi
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Fuatilia makala hii katika uchambuzi wa wachezaji waliopo Simba, Yanga, Azam ambao wanastahili kutafuta timu mpya ili kulinda viwango vya...
Fuatilia makala hii katika uchambuzi wa wachezaji waliopo Simba, Yanga, Azam ambao wanastahili kutafuta timu mpya ili kulinda viwango vyao uwanjani.

YANGA    

Kuna ugumu sana kupata nafasi ya kikosi cha kwanza kwa upande wa Yanga sababu timu imesheheni wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao hawana namba kikosi cha kwanza Yanga wanastahili kutafuta timu nyingine ili waboreshe viwango vyao.
Malim Busungu
Mmoja wa washambuliaji makini sana, alifanya vizuri sana akiwa na Mgambo JKT ya Tanga na kuivutia Yanga, ila tangu atue kwa mabingwa hao mambo yamekuwa kombo kwake amekuwa mtu wa kusugua benchi licha ya uwezo wake mkumbwa uwanjani.
Pato Ngonyani
Nafasi yake inazidi kuwa ngumu kikosini kutokana na ujio wa Vincent Andrew, uwepo wa watu makini kwenye idara ya ulinzi ya Yanga kunatoa nafasi finyu kwa kisiki huyu kucheza, anastahili kutafuta timu itakayo mpa nafasi ya kucheza kwa muda mwingi.
Matheo Anthony
Anatambulika kama Neymar wa Zanzibar, ana uwezo wa kufunga kwa mashuti ya mbali ana wakati mgumu wa kupata namba mbele ya Ngoma, Tambwe, na Chirwa ni wakati sahihi kwake kuangalia upande wa pili kutafuta timu sahihi kwake.

SIMBA    

Usajili wa wachezaji takribani 13 kwa msimu huu kunafanya baadhi ya wachezaji kuwa na wakati mgumu kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, wachezaji ambao wanaitaji kutafuta timu kulinda viwango vyao kwa upande wa Simba.
Said Ndemla
Tangu ujio wa mwalimu Mayanja kikosini maisha ya Ndemla yamebadilika si mtu wa kuanza kikosi cha Simba tena, hata mechi za maandalizi za hivi karibuni hakucheza hata mechi moja.
Dany Lyanga
Alifanya vizuri na Simba kwa msimu uliomalizika, ni mchezaji msumbufu na kasi kubwa awapo uwanjani, nafasi yake kwa sasa Simba ni ngumu kutokana na ujio wa washambuliaji wapya wenye ubora kuliko yeye.
Haji Ugando
Yupo kwenye umri sahihi wa kucheza mechi mfululizo ila kwa alipo sasa awezi pata muda mwingi wa kucheza.
Awadh Juma
Anaonekana hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu Joseph Omog, amekosekana kwenye michezo ya kirafiki ya hivi karibuni licha ya kutokuwa na majeruhi yeyote, kutokana na usajili wa wachezaji wapya ni ngumu kwake kupata nafasi.

AZAM FC    

Kama ilivyo kwa upande wa Simba na Yanga, wauza lambalamba hawa nao wamejaza rundo la wachezaji wenye vipaji benchi na hawana nafasi kwenye kikosi cha kwanza, wachezaji wanaostahili kuhama Azam na kutafuta timu kwa kuboresha vipaji vyao.
Hamiss Mcha
Amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, hata akiwa fiti bado nafasi yake imekuwa na changamoto kubwa hasa kutokana na ubora wa Singano na Farid Mussa kikosini, akiendelea kusubiri pale Azam atapoteza muda na kushusha kiwango chake.
Frank Domayo
Alikua bora alipokuwa Yanga na kupelekea Azam kushawishika kumpa mkataba, bado Domayo ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa licha ya nafasi kwenye kikosi cha Azam imekuwa ngumu kwake, ni wakati wa kutafuta timu ili kulinda ubora wake.
David Mwantika
Anapata nafasi pindi timu inapokuwa na majeruhi wengi  kwenye eneo la ulinzi, nafasi yake bado ni finyu ndani ya kikosi cha Azam licha ya uimara wake mkubwa wa kuzuia kwenye eneo la ulinzi,

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top