Unknown Unknown Author
Title: Barcelona v Atletico: Messi, Suarez dhidi ya Griezmann
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mbio za upachikaji mabao za Pichichi katika La Liga zimeshaanza na watatu kati ya wacheka na nyavu wanne Hispania. Lionel Messi, Antoin...
Mbio za upachikaji mabao za Pichichi katika La Liga zimeshaanza na watatu kati ya wacheka na nyavu wanne Hispania.
Lionel Messi, Antoine Griezmann watakabiliana usiku wa leo katika dimba la Camp Nou.
Katika mechi nne tu za ligi, bunduki hizo kubwa zimeshaanza kutunisha akaunti zao za bao na watahitaji kung'ara katika mechi yao ya kwanza yenye upinzani msimu huu.
Messi na Suarez tayari wanaujua utamu wa kunyanyua tuzo ya mfungaji bora wa msimu, lakini Griezmann hali kadhalika anao ubora wa kuwa mshindani wa kiatu hicho msimu huu.
Licha ya kuzuiwa kucheza mechi za mwanzo, Mfaransa huyo amefunga mara mbili katika mechi mbili zilizopita, na kuwafikia wadunguaji wa Barcelona.
Mchezaji wa nne ambaye naye ametisha kwa mabao hadi sasa ni Ruben Castro wa Real Betis.
Usiku wa leo tutaona, nani kati ya Mwargentina na Mfaransa atakayeendeleza moto wa mbio za kufukuzia Pichichi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top