Unknown Unknown Author
Title: Benjamin asimulia alivyokuwa wa mwisho darasani
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
September  15 2016   kupitia  Clouds 360  ya Clouds TV a mehojiwa  mtanzania  Benjamin Fernandes  mwenye   miaka 23 anayefanya kazi kweny...
September 15 2016 kupitia Clouds 360 ya Clouds TV amehojiwa mtanzania Benjamin Fernandes mwenye miaka 23 anayefanya kazi kwenye taasisi ya Melinda & Bill Gates Foundation inayoendeshwa na tajiri wa duniani, Bill Gates.
Bill Gates pia ni mwanzilishi wa kampuni ya microsoft na mbunifu mkuu wa programu za kampuni ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani.
Benjamini ameeleza namna alivyojituma licha ya kuwa na historia mbaya ya kwenye masomo darasani hapa Tanzania na alipopata nafasi ya kwenda Marekani kusoma alijituma zaidi na akawa anaongoza darasani, baadae akafanikiwa kuwa wa kwanza Afrika kushinda tuzo ya MBA/ World Summit. 
>>>’Nilisoma Kunduchi Dar ess salaam na nilivyokuwa nagraduate nikawa wa mwisho darasani hata wazazi walivyokuwa wakienda shuleni wanaambiwa huyu ni mtoto wako mbona anafeli sana mnamfundisha nini nyumbani’ Benjamin Fernandes
>>>’Nilipata nafasi moja kwenda nje kusoma waliniambia tunakupa msimu moja kwenda collage ukifaulu utaendelea na ukifanya vibaya utarudi…..Bili Gates Foundation walikuja shuleni kutafuta watu wa kufanya kazi naye, mimi nikaenda kuapply, kulikua na CV za watu 70 zikachukuliwa 20 na yangu haikuchaguliwa’ – Benjamini Fernandes
>>>Mwalimu alinishauri niende pale nikagonge mlango na niongee nao kuwa nataka kuwaona kwa dakika 5 na nilifanya hivyo:-Benjamini Fernandes
SOURCE" millady ayo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top