Unknown Unknown Author
Title: Goal inakuletea timu ya wiki baada ya mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wachezaji wa Simba na Yanga watawala kwenye kikosi bora cha wiki Ligi Kuu Tanzania Bara Goal inakuletea timu ya wiki baada ya mechi zil...
Wachezaji wa Simba na Yanga watawala kwenye kikosi bora cha wiki Ligi Kuu Tanzania Bara
Goal inakuletea timu ya wiki baada ya mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki
1.Aishi Manula- Azam
Huyu ni kipa wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania ambaye alifanya kazi kubwa ya kuiokoa timu yake Jumamosi kuepukana na kipigo kikubwa kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi licha ya kuruhusu bao moja lakini alifanya kazi kubwa ya kuzuia mashuti ya washambuliaji wa Simba anapata 1.
2. Juma Abduli - Yanga
Alikuwa kwenye ubora wake Jumamosi dhidi ya Mwadui, alipiga krosi nyingi sana za hatari na alifanikiwa kutengeneza goli la kwanza lililofungwa na Amis Tambwe anapata 2.
3.Mohamed Hussein- Simba
Alifanikiwa kuzuia mashambulizi ya Azam upande wa kulia anapo cheza Shomari Kapombe na Thomas raia wa Ivory Coast, beki huyo asiye na mpinzani mpaka sasa Ligi Kuu alikaba na kushambulia kwa wakati sahihi anapata 3.
4.Vincent Andrew- Yanga
Uwezo wake bora wa kucheza na mipira ya juu kama krosi na kona ilikuwa silaha kwa upande wa Yanga na kufanikiwa kuziba njia zote kwa washambuliaji wa Mwadui kama Paul Nonga anapata 4.
5. Mwanjale- Simba
Raia huyo wa wa Zimbabwe alifanikiwa kumficha vizuri mshambuliaji wa Azam John Bocco, aliokoa hatari nyingi langoni mwake akishirikiana na Lufungo na mechi kumalizika bila lango lao kutikiswa nyavu anapata 5.

6.Shabani Nditi- Mtibwa
Kiungo mkongwe Ligi Kuu, Nditi ndiye chachu ya ushindi wa Mtibwa dhidi ya Kagera wiki hii, aliunda ngome nzito na kuaribu mipango yote ya wapinzani, ali zuia vizuri pindi timu ilipokuwa haina mpira na kushambulia pindi walipokuwa wana mpira anapata 6.
7.Shiza Kichuya- Simba
Alifunga goli pekee kwenye ushindi wa goli moja na Azam na kuipeleka timu yake hadi kileleni mwa msimamo, alikuwa kwenye ubora wa hali ya juu na kuifanya safu ya ulinzi ya Wana lamba lamba kuwa kwenye wakati mgumu anapata 7.
8. Jonas Mkude- Simba
Jonas Mkude Licha ya kupangiwa viungo wengi kwenye pambano la Jumamosi dhidi ya Azam lakini mkude aliendelea kungara na kulitawala dimba la juu na kuwapoteza kabisa Azam huku akitengenza mipira kwa washambuliaji wake wa Simba anapata 8.
9. Donald Ngoma- Yanga
Aliwapa wakati ngumu sana mabeki wa Mwadui, alifunga Jumamosi goli moja kwenye ushindi wa goli 2 kwa bila pia alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa wenzake na kugongesha mwamba siku hiyo anapata 9.
10. Adam Kingwande- Stand United
Kiungo mshambuliaji wa Stand United ndiye mfungaji wa magoli mawili Jumapili dhidi ya JKT Ruvu kwa ushindi wa magoli mawili kwa moja anapata 10.
11. Haruna Chanongo- Mtibwa Sugar
Winga wa Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo amerudi kwenye kiwango chake cha zamani katika mchezo wa wiki hii alifunga goli moja kwenye ushindi wa magoli mawili kwa bila na Kagera anapata 11.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top