toniking toniking Author
Title: Mahakama ya Afrika kushirikiana na vyombo vya habari Tanzania
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
RAIS wa Mahakama ya Afrika, Jaji Sylvain Ore, amesema chini ya uongozi wake katika Mahakama hiyo atavipa ushirikiano vyombo vya habari vy...
RAIS wa Mahakama ya Afrika, Jaji Sylvain Ore, amesema chini ya uongozi wake katika Mahakama hiyo atavipa ushirikiano vyombo vya habari vya Tanzania, viweze kufanya kazi zao kwa uhuru huku wananchi na dunia ikipewa taarifa sahihi za mahakama hiyo.
Ore alisema hayo jana mjini hapa wakati akizungumza na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dk Jim Yonazi alipotembelea mahakama hiyo.
Alisema katika uongozi wake, atahakikisha anatoa ushirikiano kwa vyombo vya habari vya ndani kwa sababu vitaandika ukweli na kwa usahihi kuhusu kazi zifanywazo na chombo hicho, badala ya kutegemea vyombo vya nje vya kimataifa.
Alisema Tanzania ni mwenyeji wa Mahakama hiyo, ambayo iko jijini hapa, hivyo ni vyema ikatumia fursa hiyo kupitia vyombo vya habari nchini kuandika mambo yanayofanywa na chombo hicho cha maamuzi juu ya nchi za Afrika.
Ore alisema TSN kama chombo cha habari cha serikali kinapaswa kuongoza kwa kuandika habari za mahakama hiyo kwa kina kuufahamisha umma na dunia mambo yanavyoendeshwa na chombo hicho.
Rais huyo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais aliyemtangulia, Jaji Augustino Ramadhani ambaye alisema alifanya kazi nzuri katika uongozi wake tangu mwaka 2014 hadi mapema mwaka huu ndani ya chombo hicho kikubwa Afrika .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top