Unknown Unknown Author
Title: VideoFUPI: Ombi alilopokea Rais Obama kuhusu mtoto Omran wa Syria
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha ya Omran Daqdees mwenye miaka mitano ambayo alionekana akiwa na vumbi na damu baada ya nyumba yao huko Aleppo Syria kuharibiwa kati...
Picha ya Omran Daqdees mwenye miaka mitano ambayo alionekana akiwa na vumbi na damu baada ya nyumba yao huko Aleppo Syria kuharibiwa katika mlipuko, picha hiyo iliwashtua wengi duniani mwezi uliopita ikiwa ni pamoja na mvulana aitwaye Alex, ambaye anaishi Scarsdale, New York. Alex imembidi amwandikie barua President Obama ikiwa na mstari unaosema ‘atakuwa mwanafamilia mwenzetu na atakuwa kaka yetu’
Baada ya kupokea barua hiyo Rais Obama ameishare video kwenye ukurasa wake wa facebook  yenye barua hiyo na kuandika hivi…………
>>>Alex ni mtoto mwenye miaka sita. Anaishi Scarsdale, New York Marekani, mwezi uliopita kama watu wengine duniani aliguswa na taarifa za picha za mtoto Omran Daqneesh, mwenye umri wa miaka mitano huko Aleppo Syria, aliyekuwa amekaa kwenye gari la wagonjwa (Ambulance) akiwa na taharuki huku akijaribu kujifuta damu mikononi mwake.
>>>Hivyo Alex alikaa chini na kuniandikia barua, wiki hii katika mkutano wa Umoja wa mataifa uliokuwa ukijadili masuala ya wakimbizi, niliishirikisha dunia maneno mazito ya Alex.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top