Pluijm amewpongeza wachezaji wake kwa kupambana na kupata ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya wenyeji Mwadui FC
Kocha wa Yanga Hans van Der Pluijm amewpongeza wachezaji wake kwa kupambana na kupata ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya wenyeji Mwadui FC.
Pluijm ameiambia Goal, uwajibikaji wa wachezji wake umekuwa ukimpa matumaini ya kutetea tena kwa mara ya tatu taji hilo kutokana na timu nzuri aliyokuwa nayo.
"Vijana wameonyesha thamani yao ya kuwafanya kuwa wachezaji wa Yanga timu hii imekuwa ikiimarika kila msimu na ushindi wa ugenini unaonyesha namna ambavyo tunamalengo kwa misimu ijayo," amesema Pluijm.
Mabao ya Yanga katika mchezo wa jana dhidi ya Mwadui yamefungwa na Amissi Tambwe na Donald Ngoma na sasa timu hiyo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 10 sawa na Azam lakini yenyewe ikiwa imecheza mechi nne Azam na Simba wamecheza tano kila mmoja.