toniking toniking Author
Title: RC Rukwa atimua wavamizi vyanzo vya maji
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven ametoa siku 30 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Mji wa Sumbawanga (SUWASA), Idara ya Maji ya ...

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven ametoa siku 30 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Mji wa Sumbawanga (SUWASA), Idara ya Maji ya Manispaa na Ofisi ya Mkoa kushirikiana kuwaondoa wavamizi wa vyanzo vya maji katika Manispaa ya Sumbawanga.
Aliagiza hayo baada ya kutembelea chanzo kikuu cha maji cha Mto Ndua kilichopo katika kijiji cha Ulinji kinachotegemewa na wakazi wa mji wa Sumbawanga na kushuhudia shughuli za kibinadamu zikiendelea ndani ya mita 60 kutoka katika chanzo hicho cha maji ikiwemo kujenga nyumba za makazi.
Zelothe alisisitiza utekelezaji wa sheria zilizopo ili kulinda vyanzo hivyo na kuongeza kuwa watu wote watakaokamatwa wakifanya shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo vya maji wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
“Ajabu sana wananchi hao hao ambao wanaharibu vyanzo vya maji ndio wa kwanza kulalamika kuwa hawapati maji safi, sasa nitamke wazi kuwa serikali ipo na itasimamia vyanzo hivi na kuhakikisha vinalindwa kwa kutumia sheria zilizopo,” alisisitiza.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Suwasa, Hamisi Makala, chanzo cha maji cha Ndua kinaendelea kukauka na kwamba hata maji yanayopatikana sasa kwa mgao hayatoshi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top