Goal inakuletea timu ya wiki baada ya michezo ya wikendi
Goal inakuletea timu ya wiki baada ya michezo ya wikendi
1.Aishi Manula
Huyu ni kipa wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania ambaye alifanya kazi kubwa ya kuiokoa timu yake Jumamosi kuepukana na kipigo kutoka kwa JKT Ruvu ambao licha ya kuruhusu mabao mawili lakini alifanya kazi kubwa ya kuzuia mashuti ya washambuliaji wa JKT Ruvu anapata 1.
2.Ally Shomary
Mlinzi wa kulia wa Mtibwa Sugar alikuwa kwenye ubora dhidi ya Stand United licha ya klabu yake kutoibuka na alama zote tatu ile alitimiza majukumu yake kwa kiwango kikubwa
3.Mwinyi Haji
Mlinzi wa kushoto wa Yanga aliweza kumudu vyema pambano hilo ambalo liliisha kwa timu yake kushinda mchezo kwa mabao 6-2 uwanja wa Kaitaba lakini kabla ya hapo aliweza kutimiza vizuri majumu yake ikiwemo kupiga krosi nyingi ambazo washambuliaji wake walishindwa kuzitumia vizuri anapata 3.
4.Juuko Murshid
Amerudi kwenye ubora wake wa miaka ya nyuma, Mganda huyu alikuwa bora kwenye eneo la ulinzi na kufanikiwa kutoruhusu goli kwenye mchezo dhidi ya Toto Africa anapata 4
5.Agrey Moris
Beki mahiri wa Azam ambaye ameendelea kuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha kocha Zeben Hernandez alifanya kazi ya ziada ya kutoruhusu JKT Ruvu kupata goli anapata 5.
6.Jonas Mkude
Kiungo mkabaji wa Simba aliyengara kwenye kikosi cha timu hiyo kilichopata ushindi wa 3-0 dhidi ya Toto kiungo huyo aliweza kufanya kwa ufasaha kazi yake na kuwapa wakati mzuri mabeki wake wa kati anapata 6.
7.Simon Msuva
Winga mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva wikendi hii alikuwa bora sana alifunga goli moja na kutengeneza na kutengeneza magoli matatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera anapata 7
8.Muzamiru Yasin
Licha ya kupangiwa viungo watano kwenye pambano la Jumapili dhidi ya Toto lakini Muzamiru aliendelea kung’ara na kulitawala dimba la juu na kuwapoteza kabisa Toto huku akifanikiwa kufunga magoli mawili kwenye mchezo huo anapata 8
9.Obbrey Chirwa
Mshambuliaji wa Yanga ameendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 6 kwa 2 dhidi ya Kagera na yeye kufumania nyavu mara mbili anapata 9
10.Donald Ngoma
Mshambuliaji wa Yanga aliyekosa mpinzani kutokana na uwezo aliokuwa nao anapokutana na mabeki, Ngoma aliyefunga mabao mawili kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya kagera na hiyo ikiwa mara mbili mfululizo kuifunga timu hiyo tangu ajiunge na Yanga msimu huu anapata 10
11.Abdala Mfuko
Aliisaidia timu yake ya mwadui kuondoka na alama tatu dhidi ya ndanda kwenye ushindi wa magoli mawili kwa moja huku yeye akifunga magoli yote mawili anapata 11
Post a Comment