Nahodha wa Simba amefunguka kuwa timu yao imejipanga
kufanya vizuri msimu huu na hawataki mzaha huku akizitaja siri za
kiwango chao
Jumatano Novemba 2 Stand United watakuwa wenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Kambarage.
Katika harakati za kujua siri ya kiwango kikubwa cha Simba msimu huu vyombo vingi vya habari vimekuwa vikiwahoji wachezaji na wakufunzi wa timu hiyo, moja ya wachezaji waliohojiwa ni Jonas Mkude kupitia tovuti ya Shaffi Dauda.
Ikumbukwe, Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto ndio wachezaji pekee wa Simba waliovaa medali za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara Simba ilipotwaa taji hilo kwa mara ya mwisho.
Alipoulizwa nini siri ya ushindi waliopata dhidi ya timu walizokabiliana nazo Kagera Sugar na Mwadui FC Mkude alisema:
"Msimu huu tumejipanga vizuri kuanzia tulivyoanza maandalizi. Umoja uliopo kuanzia kwa mwalimu na wachezaji, viongozi na mashabiki ndio chachu ya haya yote yanayotokea."
Alipoulizwa kuhusu athari ya wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo alisema: "Siri ya wao kusajiliwa Simba lazima viongozi walikuwa wanahitaji vitu kutoka kwao, tumekaa muda mrefu bila kupata ubingwa. Wameziba mapengo ambayo waliyaona msimu uliopita yaliyosababisha sisi tukashindwa kufanya vizuri."
"Kwa falsafa ya mwalimu anaona mimi, Mzamiru na Mwinyi tunafaa kucheza pamoja wakati mwingine anaweza akaanza Mnyate au Ibrahim Mohamed. Kwahiyo mwalimu anajaribu kuchanganya watu tofauti kulingana na falsafa anayoitaka.
Post a Comment