Unknown Unknown Author
Title: Ubingwa sasa wazi baada ya Simba kupoteana Mbeya
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ambayo Jumapili iliyopita ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya African Lyon kwenye uwanja...
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ambayo Jumapili iliyopita ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru Dar ea Salaam
Mambo yamezidi kuwaendea kombo vinara wa ligi ya Vodacom Tanzania Simba baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Tanzania Prisons katika pambano lililopigwa uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ambayo Jumapili iliyopita ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru Dar ea Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35 huku Yanga wakishika nafasi ya pili na pointi zao 30 na kesho watashuka uwanjani kupambana na Ruvu Shooting ya Pwani.
Simba ambayo ilicheza bila ya yota wake wanne Ibrahim Ajibu,Fredrick Blagnon, Mohamed Ibrahim aliyeanzia benchi na Jamvier Bukungu alikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 43 na winga Jamali Mnyate aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Shizza Kichuya na ulifanya timu yake kwenda mapumziko kiongoza.
Kabla ya bao hilo Simba walicheza walionekana kuutawala mchezo na k utengeneza nafasi nyingi za mabao lakini Laudit Mavugo na na Mwinyi Kazimoto walishindwa kuzitumia.
Nahodha wa Simba Jonas Mkude nusura aifungie bao la mapema timu yake baada ya dakika ya 19 kuunganisha kwa kichwa kona ya Kichuya lakini mpira huo uliokolewa na mabeki wa Tanzania Prisons.
Lambati Sabyanka wa Prisons naye alipata nafasi nzuri dakika ya 36 lakini shuti alilopiga halikulenga lango na mpira kwenda nje ya lango na kufanya hadi mapumziko wenyeji kuwa nyuma kwa bao moja.
Kipindi cha pili wenyeji Tanzania Prisons walianza kwa kasi na iliwachukua dakika moja kupata bao la kusawazisha mfungaji akiwa ni Victor Hangaya aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Salum Kimenya.
Bao hilo lilionekana kuwapa nguvu vijana wa kocha Abduli Mingange ambao kabla ya mchezo huo walitoka kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Ndanda na Yanga Jumapili iliyopita na hawakuwa tayari kuona wanapoteza mchezo mwingine.
Hangaya aliifungia Tanzania bao la pili, alifunga tena kwa kichwa a kiunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Kimenya baada ya Pius Marcus kucheza rafu na Mohamed Husseni.
Boa hilo liliamsha nderemo za mashabi wa timu hiyo ambao walikosa furaha kwa majuma mawili kufuatia vipigo ilivyopata timu yao na kuanza kuomba nyimbo za kuwasifu wachezaji wa timu hiyo.
Kocha Joseph Omog, baada ya kuona mambo magumu aliamua kumtoa Kazimoto na kumuingiza Mohamed Ibrahim na Mussa Ndusha aliyechukua nafasi ya Nahodha Jonas Mkude aliyeinhia mnono mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Mabadiliko hayo yalionekana kuiongezea nguvu Simba na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Tanzania Prisons waliokuwa wanacheza kwa kujihami Zai baada ya wachezaji wote kurudi nyuma na kumuacha Hangaya pekeyake mbele.
Mwamuzi Endrew Shamba alikuwa mkali na kutoa kadi mbili za njano kwa wachezaji wa Tanzania Prisons kwa kosa la kupoteza muda .
Simba waliendelea kupambana kutafuta angalau sare katika mchezo huo ili kupoza machungu ya kufungwa mcheso uliopita lakini mambo yalikuwa magumu kwani Prisons hawakuwa tayari kuona wanapoteza mchezo huo tena kwenye uwanja wa nyumbani.
Mwamuzi Shamba aliongeza  dakika tano za ziada ambazo pia hazikuweza kuwasaidia vinara Simba angalau kupata sare lakini walijikuta wakimaliza mzunguko wa kwanza wakishinda michezo 11, wakitoka sare mechi mbili na kufungwa mbili.
Kwa ushindi wa leo Tanzania Prisons sasa imefikisha pointi 19 na kupanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 11 waliyokuwepo kabla ya mchezo huo wakiwa na pointi 16.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top