toniking toniking Author
Title: MICHEZO Ushindi wa Arsenal uliolinda rekodi yao ya UEFA Champions League hatua ya makundi
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
M ichuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea usiku wa Septemba 28 2016 hatua ya round ya pili, ikiwa siku moja imepita toka ichezwa baad...
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea usiku wa Septemba 28 2016 hatua ya round ya pili, ikiwa siku moja imepita toka ichezwa baadhi ya michezo ya round ya pili pia, usiku wa Septemba 28 imechezwa michezo nane ya round ya pili hatua ta makundi yaUEFA Champions League.

Mchezo wa Arsenal dhidi ya Basel ulikuwa ni moja kati ya michezo ya UEFA Champions League iliyochezwa usiku wa Septemba 28, Arsenal ambaye alikuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Emirates, aliingia katika mchezo huo akiwa na rekodi ya kucheza michezo 38 nyumbani ya mwisho ya UEFA na kupoteza mitatu pekee, akishinda 29 ns sare 6.

Hivyo Arsenal ambaye amefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Basel, goli ambazo zilifungwa na Theo Walcott dakika ya 7 na dakika ya 26, unakuwa ni mchezo wa 30 kati ya 39 Arsenal kupata ushindi katika uwanja wake wa nyumbani, licha ya Baselkuingia katika dimba la Emirates wakiwa na rekodi ya kucheza mechi 9 na kushinda yote katika Ligi Kuu Uswiss hawakuweza kutamba dhidi ya Arsenal.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top