Mchezo huu umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka kutokana na upinzani wa timu hizo mbili ulioanza tangu zilipoanzishwa miaka 80 iliyopita
Pambano la watani wa Jadi Yanga na Simba ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka linatarajiwa kupigwa kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo huo umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka kutokana na upinzani wa timu hizo mbili ulioanza tangu zilipoanzishwa miaka 80 iliyopita.
Timu hizo zinakutana zikiwa na matokeo tofauti Simba ikiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo ya Vodacom wakijikusanyia pointi 16 katika michezo sita waliyocheza wakati Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10 huku ikiwa imecheza michezo mitano mmoja nyuma ya wapinzani wao Simba.
Simba ambao watakuwa ugenini kesho wanajivunia rekoi nzuri waliyoanza nayo msimu huu ya kutopoteza mchezo hata mmoja zaidi ya sare ya 0-0 na JKT Ruvu na ushindi wa mabao 4-0, walioupata katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Majimaji niwaza utakuwa ni moja ya sababu ya kupambana ili kuendeleza wimbi lao la ushindi.
Yanga wanaingia kwenye mpambano wa kesho wakiwa wanatoka kupoteza mchezo wao wa mwisho kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage matokeo hayo niwazi yatakuwa hayaja wafuraisha na wataingia kwenye mchezo wa kesho kwa nguvu kutaka kusawazisha makosa yao.
Kocha Hans van der Pluijm amesema vijana wake wote wapo tayari na amewapangia Simba kikosi ambacho kitamaliza mchezo huo mapema kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Pluijm anasema kupoteza mchezo wa Stand United kusiwape matumaini ya ushindi Simba kwani wamepanga kuingia kwa kasi wakilishambulia lango la Simba na kuhakikisha wanapata mabao mawili ya haraka yatakayo wachanganya vijana wa kocha Joseph Omog.
Nguvu kubwa Yanga katika mchezo wa kesho ni uimara wa safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Donald Ngama na Amiisi Tambwe ambao kwa pamoja wameshafunga mabao manne katika mecho zote tano walizocheza msimu huu.
Kasi ya viungo Simon Msuva na Deusi Kaseke inaweza kuwa msaada mkubwa kwa Thabani Kamusoko ambaye kazi yake katika mchezo huo itakuwa ni moja kusambaza mipira kwa washambuliaji wake Ngoma na Tambwe ili waweze kupata mabao hayo.
Ingawa Kamusoko mechi iliyopita alicheza chini ya kiwango lakini hiyo ilitokana na ubovu wa kiwanja cha Kambarage ambacho kina utofauti mkubwa na ule wa taifa hivyo viungo wa Simba watarajie kupata usumbufu mkubwa wa kumdhibiti kiungo huyo bora wa kimataifa msimu uliopita.
Kocha Pluijm huenda akaanza kutumia mpfumo wa 4-3-3 kwa ajili ya kujaza watu wengi kwenye eneo la kiungo ili kuzuia Simba kwenye eneo lao la kiungo wa chini ambalo kidogo linaonekana kuwa dhaifu lakini watakuwa na kazi ya kupanda na kuwa wengi pindi wanapofanya mashambulizi kwenye lango la Simba.
Tambwe na Ngoma wataendelea kuwa wachezaji wa kuchungwa na safu ya ulinzi ya Simba kutokana na uwezo waliokuwa nao pindi wanapoachiwa nafasi na beki Method Mwanjali huenda thamani yake na uwezo wake halisi ukaonekana hapo kama ataweza kuwazuia Yanga wasimfunge kipa wake Agnban.
Simba ndiyo iliyopania zaidi kushinda mchezo wa kesho ikiwa na sababu zisizo pungua tatu kwanza wanataka kulipa kisasi cha kupoteza mechi zote mbili za msimu uliopita, pili ni kuonyesha ubora waliokuwa nao kwa kutumia wachezaji wapya iliyo wasajili msimu huu na mwisho ni watataka kuendeleza rekodi yao ya ushindi ili kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Nikweli kwamba Simba ya msimu huu inamabadiliko makubwa tofauti na ile ya msimu uliopita, na ujio wa kocha Joseph Omog umeonyesha tofauti kubwa na kuirudisha timu hiyo kwenye mbio za ubingwa na klabu za Azam na Yanga tofauti na ilivyokuwa huko nyuma sasa timu hiyo inaonyesha inatafuta matokeo gani inapokuwa uwanjani.
Simba imekuwa imara sana kwenye eneo la kiungo na inajivunia zaidi safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Laudi Mavugo, Ibrahim Ajibu na Shizza Kichuya ambao wote kwa pamoja wamefunga mabao tisa katika mechi walizocheza msimu huu hivyo kama wanakutana na timu yenye beki dhaifu nivigumu kuidhibiti kasi yao.
Ajibu amekuwa na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake wa mbele na staili yake ya kurudi kati kuchukua mipira na kupanda nayo kwenye eneo la wapinzani wao kunaweza kuidhuru Yanga kama kwenye eneo la kiungo mkabaji watamtumia mkongwe Mbuyu Twite.
Mara nyingi asilimia kubwa ya mabao ya Mavugo yametokana na pasi za Ajibu au beki wao wa kushoto Mohamed Hussein hivyo niwazi katika mchezo hu safu ya ulinzi ya Yanga inatakiwa kuwa makini kuwadhibiti nyota hao.
Sehemu nyingine ambayo Simba wanaonekana kuwa vizuri ni upande wa mawinga Shizza Kichuya na Jamali Mnyate hawa ni watu hatari wenye kasi na mara zote huchukulia mipira pembeni na kuingia nayo kwenye eneo la hatari kama walizinzi wa Yanga wasipokuwa makini wanaweza kusababisha penati vinginevyo wanapaswa kumalizana huko huko pembeni.
Tatizo kubwa la Simba ambalo wanatakiwa kuwa makini ni sehemu yao ya ulinzi hadi kwenye kiungo wa chini namba 6 ambao ltayari hadi sasa katika mechi sita walizocheza wameruhusu mabao mawili na tatizo lao kubwa ni kupiga pasi fupi futi ambazo zinaweza kuwa na madhara kwao kutokana na ushapu waliokuwa nao washambuliaji wa Yanga.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Omog kukutana na Yanga akiwa kama kocha wa Simba na anatarajiwa kutumia mfumo wa 4-4-2 ambao amekuwa akiutumia kwenye michezo yote iliyopita na kumpa ushindi uliomfanya aongoze ligi.
Post a Comment