Simba na Stand United ndiyo klabu pekee ambazo hazijapoteza mechi mpaka sasa msimu huu baada ya michezo saba kwenye Ligi Kuu Bara
Ligi kuu Tanzania Bara  ipo mzunguko wa saba, Mnyama Simba ikiwa kileleni kwa alama 17, Stand United na Mtibwa wanashika nafasi ya pili na tatu huku bingwa mtetezi Yanga yupo wa tano kwenye msimamo kwa alama 11 alizokusanya.
Goal inakuletea kikosi cha wachezaji 11 tangu mzunguko wa kwanza hadi sasa
1.Said Kipao
Amecheza mechi 6 ameruhusu magoli 3 pekee sawa na klabu ya Simba , kipao licha ya kucheza JKT Ruvu ameonesha ubora mkubwa kwenye kulinda lango lake.
2.Juma Abduli
Amehusika kwenye mabao 3 kwenye magoli 9 yanga waliyofunga, ndiye beki wa kulia aliye changia magoli mengi mpaka sasa uwezo mkubwa wa kushambulia na kupiga krosi kumezidi kuleta faida ndani ya klabu.
3.Mohamed Hussein
Ndiye mlinzi aliyetoa pasi nyingi za magoli kwenye Ligi Kuu, amehusika kwenye magoli 5 ndani ya klabu ya Msimbaz alihusika kwenye mechi dhidi ya Ndanda pasi tatu, Mtimbwa na Majimaji.
4.Erick Mulilo
Ni Simba na Stand United ndiye klabu pekee ambazo hazijapoteza mechi mpaka sasa, Mulilo amefanikiwa kuunda safu ngumu ya ulinzi na kuifanya chama la Wana kuwa ni moja ya timu ngumu kufungikwa, wameruhusu magoli matatu tu goli moja nyuma ya Yanga aliyefungwa magoli 2.
5.Method Mwanjali
Amecheza takribani dakika 630 bila kutetereka na kufanikiwa kulinda rekodi yao ya kutopoteza kwa msimu huu.
6.Shabani Nditi
Kiungo mkongwe Ligi Kuu Bara bado anaonesha uhai ndani ya Mtibwa licha ya umri kwenda, amefanya kazi kubwa mpaka sasa kwa kukaba na kuilinda safu yake ya ulinzi vizuri licha ya kuondokewa na wachezaji wengi msimu huu ila kiungo huyo ameendeleza ubora wake wa siku zote.
7.Shiza Kichuya
Ndiye mchezaji bora Ligi Kuu mpaka sasa, Kichuya amecheza mechi saba na kufunga goli tano na kukaa juu kwenye kinyang’anyiro cha ufungaji bora hali kadhalika ameonesha uwezo mzuri kwenye kutengeneza nafasi kwa wenzake.
8.Thabani Kamusoko
Amekuwa akicheza maeneo tofauti tofauti msimu huu kulingana na mpinzani watakaye cheza naye, Kamusoko ametoa pasi 2 za goli kwenye michezo 6.
9.Amis Tambwe
Mfungaji bora wa msimu uliomalizika ameanza msimu kwa kasi kubwa amefunga magoli 4 katika mechi 6 na kutoa pasi ya goli moja anazidiwa goli moja na kinara wa mabao Shiza Kichuya .
10. Raphael Daud
Kwa mechi saba tu tayari ameanza kuzivutia klabu kubwa hapa nchini, kiungo huyo mshambuliaji amefunga magoli matatu hadi sasa, ameonesha uwezo mkubwa hasa akicheza nyuma ya mshambuliaji.
11.Ibrahim Ajibu
Amekuwa na mchango mkubwa kuifanya Simba kukaa kileleni mwa msimamo, Ajibu siye mzuri kwenye kufunga tu bali ni mzuri kwenye kutengeneza nafasi za magoli.