Unknown Unknown Author
Title: Cristiano Ronaldo afanya kufuru kwa kupiga hat-trick yake ya 42
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Supastaa wa Real Madrid amerejea kwenye timu yake ya taifa kwa hasira kali na kuiadhibu Andorra katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 20...
Supastaa wa Real Madrid amerejea kwenye timu yake ya taifa kwa hasira kali na kuiadhibu Andorra katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018
Cristiano Ronaldo amefunga magoli manne wakati Ureno wakitoa kichapo cha magoli 6-0 dhidi ya Andorra kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Ronaldo alifunga magoli mawili, moja kwa kichwa jingine kwa mguu ndani ya dakika nne za kipindi cha kwanza na kuwaweka mbele mabingwa wa taji la Euro 2016.
Joao Cancelo aliongeza bao la tatu kisha Ronaldo akafunga goli lake la tatu kukamilisha hat-trick yake katika mchezo huo.
Ronaldo alirejea kambani kwa mara nyingine kufunga goli lake la nne katika mchezo huo huku likiwa ni goli la tano kwa Ureno kabla ya Andre Silva kuhitimisha karamu ya magoli dhidi ya Andorra ambao walipoteza wachezaji wao wawili kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu.
Ureno kwa sasa wapo nafasi ya tatu katika Kundi B wakiwa wamepoteza mchezo dhidi ya vinara wa kundi hilo Switzerland ambao wameifunga Hungury 3-2 kwenye mchezo wao wa Ijumaa.
Hat-trick hiyo inamfanya Ronaldo aweke rekodi ya kufikisha jumla ya hat-trick 42 katika maisha yake yote ya soka.
Ronaldo alipata majeraha kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2016, mchezo dhidi ya Andorra ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza wa kimataifa tangu fainali ya Euro ambapo Ureno ilishinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top