Unknown Unknown Author
Title: Hasira na Faida za Kukodishwa Yanga
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Goal inakuletea faida na hasara inazoweza pata Yanga baada ya kukodisha timu Bodi ya wadhamini ya klabu ya Yanga imesaini mkataba wa ...
Goal inakuletea faida na hasara inazoweza pata Yanga baada ya kukodisha timu
Bodi ya wadhamini ya klabu ya Yanga imesaini mkataba wa kuikodisha timu yao kwa kampuni ya Yanga Yetu Limited chini ya bwana Yusuph Manji kwa kipindi cha miaka 10
Yanga Yetu Limited ni Kampuni iliyoundwa ili iweze kuingia katika Mkataba na YANGA ili iweze kutimiza malengo ya klabu kama yalivyoazimiwa katika Mkutano wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016.
Ni jambo zuri kwa klabu kama ya Yanga kujiendesha kisasa na kuachana na sera za kizamani licha ya huo mfumo kutarajiwa kuwa na changamoto nyingi kwani ni mpya kutumika kwenye medani za soka huku mfumo uliozoeleka ni hule wa klabu kuuza hisa zake kwa makampuni na wanachama
Kwa takribani miaka 80 klabu Yanga imekuwa ikijiendesha kwa hasara huku kwa asilimia kubwa  ikitegemea michango kutoka kwa wahisani na mikopo kutoka kwa baadhi ya wanachama na makampuni ili kujiendesha 
Goal inakuchambulia faida watakazo pata klabu ya Yanga kama mkataba utazingatiwa vizuri 
Kuimarika kwa matawi ya Yanga 
Kifungu cha 3.2 kinazungumzia” mkodishwaji atailipa Yanga milioni 100 huku asilimia 90 ya fedha yote itaenda kuimarisha mtandao wa matawi kote nchini” hivyo matawi ya klabu ya Yanga yatakuwa na nguvu ya kujiendesha bila kutegemea michango midogo midogo ya wanachama
Kuimarika kwa miundo mbinu
Na katika namna zote mbili hapo juu.Yanga SC itavuna faida ya 25% bila Yanga SC kuwekeza mtaji wowote bali thamani ya nembo na jina lake tu kwa hiyo asilimia 25 itatumika kuimarisha na kujenga miundo mbinu kama viwanja na hostel.
Klabu itaweza kushindana kikamilifu katika shughuli za mpira ndani na nje ya nchi
Katika uendeshaji wa klabu na haitaumiza kichwa kuhusu usajili,mishahara wala huduma yoyote kwa timu, pia ndani ya mkataba huo unazungumzia juu ya uundwaji wa timu ya vijana kulingana na kanuni za TFF kifungu namba (3.9) na (3.12) hivyo itafanya klabu kuzalisha wachezaji wengi na bora kwa kipindi chote halikadharika kuifanya kuwa moja ya klabu bora Afrika kulingana na wingi la vijana watakao zalisha
Hali kadhalika goal inakuletea hasara zinazoweza kupatikana 
Kuiacha klabu tegemezi baada ya mkataba kuisha
Kwa hali ilivyo bila shaka klabu itarudia tena kwenye utegemezi wa wanachama na michango ya wahisani baada ya mkataba wa miaka kumi ya mkataba  kuisha
Klabu haitakuwa na nguvu ya moja kwa moja kuingia kwenye mikataba na makampuni mengine
Mkodishwaji ndiye mwenye nguvu kubwa ndani ya klabu ana uwezo wa kusaini mikataba mbali mbali na kampuni tofauti tofauti bila klabu kuwa na mchango wa moja kwa moja

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top