Baraza la Michezo Tanzanzani (BMT) limezitaka klabu za soka nchini kufuata sheria na taratibu sahihi kabla ya kufanya mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja ameiambia Goal, wanatambua kuwa vilabu vinavyotaka kufanya mabadiliko vina malengo ya kupata mafanikio na kama baraza linabariki mafanikio hayo lakini lazima taratibu za zifuatwe ikiwa ni pamoja na wanachama wao kupata fursa ya kujadili jambo linalotaka kutokea kwenye klabu yao pamoja na kupata ufafanuzi pale inapobidi sambamba na kupatiwa elimu juu ya faida na hasara za mifumo husika.
“Hili nalisema hususani kwa klabu hizi kongwe za Simba na Yanga ambazo ndiyo zipo katika mchakato wa kubadilisha uendeshwaji wao yasije baadaye huko mbele pakatokea vurugu na malubano kwasababu tu wanachama na mashabiki hawana uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko hayo,”amesema Kiganja.
Klambu za Simba na Yanga zipo katika mchakato wa kufanya mabadiliko huku Kiganja akisisitiza ni lazima sheria na taratibu zifuatwe ili kutawapa mamlaka ya kufanya mabadiliko hayo.
Post a Comment