toniking toniking Author
Title: Nyangumi akutwa amekufa ufukweni
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
SAMAKI Mkubwa aina ya Nyangumi amekutwa leo akiwa amekufa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoa...
SAMAKI Mkubwa aina ya Nyangumi amekutwa leo akiwa amekufa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Ripiti kutoka eneo la tukio zinasema Nyangumi huyo alianza kuonekana akielea baharini tangu jana na leo alfajiri alisukumwa hadi ufukwe huo katika bandari ya wavuvi.
Mmoja wa wananchi katika eneo hilo, Akram Kidudu ameiambia Habarileo Online kuwa bado haijajulikana chanzo cha kifo cha nyangumi huyo na polisi wapo eneo la tukio kuzuia wananchi wasianze kugawana kitoweo hicho bila kujua usalama wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top