Unknown Unknown Author
Title: Hatuna mpango wa kubadilisha kocha" - Boniface Mkwasa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkwasa amesema hawana mpango wa kumtimua kocha wao Mzambia George Lwandamina, ili kumleta Stewart Hall Katibu mkuu ya  Yanga  Bonifac...
Mkwasa amesema hawana mpango wa kumtimua kocha wao Mzambia George Lwandamina, ili kumleta Stewart Hall
Katibu mkuu ya Yanga Boniface Mkwasa amesema hawana mpango wa kumtimua kocha wao Mzambia George Lwandamina, ili kumleta Stewart Hall.
Mkwasa ameiambia Goal, wanaimani kubwa na Lwandamina na wataedelea kuwa naye hadi mkataba wake utakapomalizika Mei 2019.
“Kama uongozi tuna imani kubwa na kocha wetu pamoja na benchi zima la ufundi kifupi hatuna mpango wa kubadilisha kocha na wala hatujazungumza chochote na Hall bado tuna imani na benchi letu la ufundi,” amesema Mkwasa.
Katibu amesema kwa kiwango ambacho timu yao inakionyesha wameridhika kabisa na kiwango chake na pia hawataki kubadilisha kocha kwa kuhofia kuwachanganya wachezaji wao kipindi hiki ambacho wanawania ubingwa wa ligi ya Vodacom.
Amesema wakiwa na Lwandamina wanaamini wanauwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi ya Vodacom pamoja na Kombe la FA, lakini pia kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hapo mwakani.
Katika hatua nyingine Mkwasa, amesema maandalizi kwa ajili ya mchezo dhidi ya MC Alger, yanaendelea vizuri na wana matumaini makubwa kushinda mchezo huo uliopangwa kupigwa Jumamosi ijayo.
Amesema timu yao chini ya Lwandamina imeendelea kujifua uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini na wanauhakika kupata huduma ya mshambuliaji Donald Ngoma ambaye ameanza mazoezi siku mbili zilizopita.
Amesema wanataka kumaliza mchezo huo kwa kupata ushindi mnono wa mabao 3-0, ili kuwa na kazi rahisi kwenye mchezo wa marudiano ambao utachezwa Algeria Aprili 14.
“Lengo letu ni kucheza hatua ya makundi na hilo linawezekana kutokana na hali ya kuimarika kwa kiwango chetu katika kila mchezo ukiangalia hivi sasa tumerudi kileleni kwenye ligi ya Vodacom tunaimani pia tutashinda mchezo wetu wa nusu fainali wa Kombe la FA,”amesema Mkwasa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top