Unknown Unknown Author
Title: "Kilichotokea ni miujiza" - Joseph Omog
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha huyo amesema ameshukuru kuona wachezaji wake walifanya kile alichowaelekeza Kocha Mkuu wa  Simba  Joseph Omog, amesema ushindi ...
Kocha huyo amesema ameshukuru kuona wachezaji wake walifanya kile alichowaelekeza
Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog, amesema ushindi walioupata jana ulitokana na miujiza ya Mungu kwani alishakubali kupoteza mchezo huo mbele ya Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Omog ameiambia Goal, vijana wake walicheza kwa juhudi kubwa hadi kupata ushindi huo wa mabao 3-2, na anampongeza sana mshambuliaji Fredrick Blagnon ambaye alitokea benchi na kwenda kubadilisha matokeo ya mchezo huo zikiwa zimebaki dakika nane mchezo kumalizika.
“Ukweli kama nimeishiwa maneno siamini kilichotokea nahisi ni miujiza ya Mungu tu, vijana wangu walicheza vizuri baada ya kutanguliwa mabao mawili na wenyeji wetu Mbao, lakini kipindi cha pili niliwataka wachezaji wangu wasikate tamaa na kupandisha mipira mbele angalau tupate hata bao moja,” amesema Omog.
Kocha huyo amesema ameshukuru kuona wachezaji wake walifanya kile alichowaelekeza lakini baada ya kuona hadi dakika ya 80 hawajapata bao mambo yalikuwa magumu lakini nawapongeza wachezaji kwa juhudi walizozionyesha.
Amesema ushindi huo kwasasa umefufua matumaini yao ya ubingwa na watahakikisha wanapambana katika mechi zilizo salia ili kuhakikisha wanatimiza lengo lao la ubingwa msimu huu.
Amesema baada ya mchezo huo hawatofanya makosa tena ya kujaribu baadhi ya wachezaji kitu ambachi kiliwasumbua hata kutanguliwa kufungwa mabao mawili hapo jana na wenyeji wao Mbao FC.
Simba kwasasa wamerejea kileleni wakiwa na pointi 58, na kuishusha Yanga kwenye nafasi ya pili wakibakiwa na pointi zao 56 lakini wakiwa na mchezo mmoja nyuma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top