Mchezo huo licha ya kuisha kwa sare ya kufungana 1-1, lakini uligubikwa na vurugu kubwa hasa baada ya Yanga kupata bao la kwanza lililofungwa na Amisi Tambwe
Waziri Nape ameiambia Goal, kwamba hawato zipa klabu hizo mapato ambayo yamekusanywa kwenye mchezo huo na badaya yake watatumia pesa hizo kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya uwanja huo ambayo imeharibiwa na mashabiki wa pande zote mbili.
“Kama Serikali hatuwezi kuvumilia upuuzi huu nivyema tukawapa nafasi watu wengine wastaarabu ambao wanaweza kuutumia uwanja huu na siyo Simba na Yanga ambao wamevunja mageti manne mawili upande wa Yanga na mawili mengine upande wa Simba lakini pia viti vipatavyo 1,781 vimengolewa na mashabiki wa Simba,”amesema Waziri Nape.
Mchezo huo licha ya kuisha kwa sare ya kufungana 1-1, lakini uligubikwa na vurugu kubwa hasa baada ya Yanga kupata bao la kwanza lililofungwa na Amisi Tambwe ambaye inadaiwa kabla ya kufunga bao hilo aliushika mpira.
Post a Comment