Picha lilivyojitengeneza
Magoli mawili ya Laudit Mavugo kwenye mchezo wa Kundi A dhidi ya Jang’ombe Boys yameifanya Simba kufikisha pointi 10 na kuwa kinara wa kundi hilo kwa sababu timu yoyote itakayoshinda mchezo wa saa 2:15 kati ya URA na Taifa Jang’ombe haiwezi kufikisha pointi hizo.
Yanga baada ya kusukumwa goli 4-0 na Azam FC kwenye mchezo wa jana usiku, wakajikuta wanamaliza katika nafasi ya pili kwa pointi zao sita nyuma ya Azam yenye pointi saba.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, kinara wa kundi A anakutana na mshindi wa pili kutoka Kundi B wakati Kinara wa Kundi B yeye anakutana na timu iliyoshika nafasi ya pili katika Kundi A na hapo ndipo mechi ya Simba na Yanga inapozaliwa.
Post a Comment