Unknown Unknown Author
Title: EXTRA TIME: Kagera Sugar wamchongea Abdi Banda kwenye kamati ya masaa 72
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa ushindi wa wikendi iliyopita, Kagera wanafanikiwa kumshusha Azam nafasi ya tatu kwa alama zao 45 kwenye michezo 25 Klabu ya Kager...
Kwa ushindi wa wikendi iliyopita, Kagera wanafanikiwa kumshusha Azam nafasi ya tatu kwa alama zao 45 kwenye michezo 25
Klabu ya Kagera Sugar imesikitishwa na ukimya wa kamati ya masaa 72 kuhusu sakata la Abdi Banda wa Simba la kumpiga ngumi mchezaji wao George Kavila katika mchezo  wa Ligi Kuu uliowakutanisha siku ya Jumapili iliyopita.
Kupitia akaunti yao ya instagram ya Kagera Sugar @kagerasugar, wameshangazwa na kamati hiyo ya masaa 72 kutozungumza chochote kuhusu kitendo cha mlinzi wa Simba, Abdi Banda kuonekana akimpiga ngumi  kwa makusudi kapteni wao George Kavila kwenye harakati za kugombania mpira.
Kadhalika Kagera Sugar wamewataka wadau wote wa soka nchini kuungana na kuukemea uhuni huo aliyo ufanya Banda.
"Za hasabuhi wadau hivi ile kamati ya saa 72 bado haijasema chochote kuhusu hili vipi mbona wadau wengine hawapazi sana sauti kuhusu hili au kwa sababu limefanywa na moja ya pacha wa kariakoo??? Vp muhusika hata radhi hajaomba? Ok wacha tuendelee kusubiri pole sana capteiiiin@georgekavila".
Katika mchezo Kagera Sugar walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya Mnyama Simba, shukrani kwa magoli ya Mbaraka Yusuph na Edo Christopher huku lile la kufutia machozi la Wekundu wa msimbazi likifungwa na kiungo wa Mzamiru Yassin.
Kwa ushindi wa wikendi iliyopita, Kagera wanafanikiwa kumshusha Azam nafasi ya tatu kwa alama zao 45 kwenye michezo 25 alama moja nyuma dhidi ya Waoka mikate hao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top