Unknown Unknown Author
Title: AZAM FC WILL FACE MAJIMAJI,
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya kuponea chupuchupu na aibu ya kipigo kutoka kwa African Lyon Jumamosi iliyopita kikosi cha Azam chini ya kocha Zeben Hernandez, ...
Baada ya kuponea chupuchupu na aibu ya kipigo kutoka kwa African Lyon Jumamosi iliyopita kikosi cha Azam chini ya kocha Zeben Hernandez, kesho Jumamosi kitakuwa na nafasi ya kurekebisha makosa yake wakati kitakapoialika Majimaji ya Ruvuma kwenye uwanja wake wa Azam Complex Chamaz.
Timu hizo zinakutana wakati ambao Azam wakipewa nafasi kubwa ya kushinda kwani rekodi inaonyesha Majimaji hawajawahi kupata ushindi mbele ya Azam katika mechi zote mbili walizowahi kukutana.
Majimaji ambayo inanolewa na kocha Hassan Banyai, ilipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons wakiwa nyumbani uwanja wa Majimaji hivyo wana kazi kubwa kuhakiksha wanapata pointi tatu wakiwa ugenini mbele ya Azam ambayo nayo inahitaji ushindi ili kufufua matumaini yao.
Kocha Hernandez amesema baada ya matokeo mabaya ya mchezo uliopita timu yake imeendelea kuimarika na ana uhakika wanaweza kupata ushindi katika mchezo wao wa kesho kwa sababu wachezaji wake wameonyesha kushika vizuri mafundisho ambayo amekuwa akiwapa mazoezini.
“Tumezidi kuimarika, na hata makosa tuliyoyafanya kwenye mchezo wetu wa kwanza tumeyarekebisha na ninaamini hayatajirudia tena tunahitaji ushindi na hilo ndiyo jambo jema hasa tunapokuwa nyumbani mbele ya mashabiki wetu,” amesema Hernandez.
Kocha huyo amesema ataendelea kumtumia nahodha wake John Bocco, kwa kuwa yupo kwenye kiwango bora hivi sasa pamoja na beki wake Shomari Kapombe ambaye ameendelea kufanya vizuri tangu arejee uwanjani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top