Unknown Unknown Author
Title: Bayern Munich v Werder Bremen: Carlo Ancelotti ataanzaje
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya kuisubiri kwa muda wa miezi mitatu, hatimaye Bundesliga inarejea tena. Msimu unaanza kwa mechi kubwa kati ya mabingwa watetezi F...
Baada ya kuisubiri kwa muda wa miezi mitatu, hatimaye Bundesliga inarejea tena. Msimu unaanza kwa mechi kubwa kati ya mabingwa watetezi FC Bayern dhidi ya Werder Bremen.
Wageni wa mchezo huo katika dimba la Allianz Arena wanaweza sasa wasiwe na nguvu kama ambavyo walikuwa kipindi wanashinda ubingwa mwaka 2004, lakini kikosi cha Viktor Skripnik bado wanategemewa kutoa ushindani mkubwa kwa Carlo Ancelotti ambaye atakuwa anaiongoza Bayern kwa mara ya kwanza katika Bundesliga.
Muitaliano huyo tayari ameshaanza na mwanzo mzuri kwa kushinda Taji la Ujerumani Super Cup na mchezo wa kwanza wa DFP Cup, lakini malengo makubwa ya klabu yapo katika Bundesliga – “Malengo yetu makuu ni kushinda ligi,” Ancelotti alisema wakati anawasili na kuanza kwa ushindi wa pointi 3 kesho Ijumaa itakuwa ni msingi mzuri kuelekea kutimiza malengo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top