toniking toniking Author
Title: Serengeti Boys yanusa fainali
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
SERENGETI Boys imebakisha kikwazo kimoja kabla ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, b...
SERENGETI Boys imebakisha kikwazo kimoja kabla ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, baada ya kuifunga Afrika Kusini 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Baada ya ushindi huo wa jana, Serengeti Boys sasa itacheza na mshindi wa mchezo wa Congo Brazzaville na Namibia kabla ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Madagascar mwakani.
Serengeti Boys iliandika bao la kuongoza katika dakika ya 35 lililofungwa na Mohamed Abdallah baada ya kupata krosi ya Yohana Mkomola. Muhsin Makame aliihakikishia ushindi Serengeti Boys pale alipofunga bao la pili katika dakika ya 84 baada ya pasi nzuri ya Mohamed Abdallah.
Serengeti Boys ilipata pigo pale mchezaji wake, Ally Ng’azi alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Bonga Dladla.
Awali, Serengeti Boys ndio ilikuwa ya kwanza kuliweka majaribuni lango la wapinzani wao baada ya Mohamed Abdallah kushindwa kufunga katika dakika ya tatu licha ya kuwa katika nafasi nzuri kwani alipiga mpira nje.
Wenyeji nusura wafunge katika dakika ya 14 wakati Kelvin Naftal alipokuwa katika nafasi nzuri lakini kabla hajaleta madhara, mabeki wa Afrika Kusini waliokoa hatari hiyo.
Kocha wa Serengeti Bakari Shime `Mchawi Mweusi’ aliipongeza timu yake kwa ushindi huo na kusema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kuliko ule wa awali, ambao timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1 Afrika Kusini na kuifanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.
Kikosi cha Serengeti Boys: Ally Msengi, Ramadhani Kabwili, Nickson Job, Israel Mwenda, Ally Ng’azi, Kelvin Naftal, Shaban Ada, Mohamed Abdallah, Yohana Mkomola na Asad Juma/Issa Makamba

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top