Unknown Unknown Author
Title: Aliyeigiza Liesl The Sound of Music Charmian Carr afariki dunia
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Carr amefariki akiwa mjini Los Angeles baada ya kupata matatizo kutokana na aina nadra ya ugonjwa wa dementia, mwakilishi wake amesema. ...
Carr amefariki akiwa mjini Los Angeles baada ya kupata matatizo kutokana na aina nadra ya ugonjwa wa dementia, mwakilishi wake amesema.
Akiigiza kwenye filamu hiyo maarufu sana ya mwaka 1965, alisifika kwa alivyoimba wimbo wa Sixteen Going on Seventeen.
Baada ya kuondoka kwenye ulingo wa filamu, alianzisha biashara ya kupamba nyumba katika jimbo la California.
Mamake ndiye aliyempangia kwenda kushindania nafasi ya kuigiza Liesl, ingawa hakuwa amepokea mafunzo ya uimbaji au uigizaji.
Filamu hiyo ya The Sound of Music iliyondaliwa na Rodgers na Hammerstein ilivuma sana, na iliipiku filamu ya Gone with the Wind wakati huo na kuwa filamu iliyozoa kitita kikubwa zaidi cha pesa katika historia kufikia wakati huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top