Unknown Unknown Author
Title: Arsenal vs Chelsea: Wenger anataka kufuta gundu la kushindwa kuifunga Chelsea
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Arsene Wenger atakuwa katika harakati za kuhitimisha mwendo wa mechi tisa bila ya ushindi dhidi ya Chelsea akiwa na Arsenal Wiki hii ...
Arsene Wenger atakuwa katika harakati za kuhitimisha mwendo wa mechi tisa bila ya ushindi dhidi ya Chelsea akiwa na Arsenal
Wiki hii Arsene Wenger anasherehekea kutimiza miaka 20 tangu alipotangazwa kuwa meneja wa Arsenal, atakabiliana na timu ambayo amekuwa na uhasama nayo sana Chelsea.
Mfaransa huyo anatumai kuweka kumbukumbu yake ya miaka 20 kwa ushindi lakini timu yake imeshindwa kupata ushindi dhidi ya Chelsea katika mechi tisa walizokutana Ligi Kuu Uingereza na miamba hao wa Darajani Stamford.
Kwa hakika, Arsenal pia wameshindwa kufunga katika mechi zao sita za mwisho za ligi dhidi ya Chelsea lakini ushindi hapa unaweza kuwapa ushindi wa nne mfululizo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.
Conte ndiye atakayesimama kidete kushindana na Wenger, akiwa anataka kukwepa kupoteza mechi ya tatu Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu alipopata sare nne mfululizo akiwa na Juventus Machi 2012.
Habari za Timu
Arsene Wenger atawarejesha wachezaji wake wa siku zote katika kikosi cha kwanza kwa mechi ya Jumamosi nyumbani dhidi ya Chelsea.
Bosi huyo wa Gunners alifanya mabadiliko 11 Jumanne usiku katika ushindi wa Kombe la EFL dhidi ya Nottingham Forest, lakini wachezaji kama Petr Cech, Laurent Koscelny, Mesut Ozil na Alexis Sanchez watarejea mzigoni katika uwanja wa Emirates.
Olivier Giroud (jeraha la dole gumba) atafanyiwa vipimo dakika za mwisho kabla ya mchezo, wakati Aaron Ramsey (majeraha ya misuli), Per Mertesacker, Danny Welbeck na Carl Jenkinson (wote wakisumbuliwa na goti) watakuwa nje ya mchezo huu.
Chelsea bado wataendelea kuikosa huduma ya John Terry. Nahodha huyo na beki wa kati anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata katika sare ya 2-2 dhidi ya Swansea, licha ya faraja na imani kuwa angepona haraka.
Ilitarajiwa kuwa yeye na beki mwenzake wa kati, Kurt Zouma ambaye ni majeruhi pia, wangerejea mazoezini mapema.
Lakini pamoja na yote hayo, Antonio Conte bado anacho kikosi kipana cha kuchagua wachezaji anaowataka na atalazimika kuamua kumchezesha Cesc Fabregas dhidi ya timu yake ya zamani baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Leicester au la!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top