Unknown Unknown Author
Title: Mashetani au Mbweha? Manchester United dhidi ya Leicester
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza Leicester City watasafiri kwenda Old Trafford Jumamosi kuikabili Manchester United mchana. Mbeha hao &...

Mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza Leicester City watasafiri kwenda Old Trafford Jumamosi kuikabili Manchester United mchana.
Mbeha hao "Foxes" watakuwa wakitafuta nafasi ya kulipa kisasi kwa Mashetani Wekundu baada ya timu hiyo ya Jose Mourinho kushinda Ngao ya Jamii mwezi Agosti.
Mashetani Wekundu wamepoteza mechi zao mbili za nyumbani lakini ushindi wa 3-1 dhidi ya Northampton ulidhihirisha kuwa timu hiyo ya Old Trafford imerejea kwenye njia za ushindi kuelekea mechi ya Jumamosi saa 8:30 mchana.
Mechi Muhimu kwa Wayne Rooney
Macho ya wengi yapo kwa Rooney, ambaye kiwango chake hakiridhishi. Kuna hati hati akakosa namba kikosi cha kwanza katika mechi ya Jumamosi.
Nahodha huyo wa United, 30 amefunga mara moja tu msimu huu na kiwango cha Marcus Rashford kinazidi kumpa presha katika nafasi yake kikosi cha kwanza.
Mashabiki wa United wamechoshwa na kiwango dhaifu kinachooneshwa na nahodha wao - hali kadhalika matokeo duni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top