Unknown Unknown Author
Title: Mourinho: Makosa ya mwamuzi yameiadhibu United
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amelaumu makosa ya yaliyofanywa na mwamuzi Michael Oliver kwa kipigo cha 3-1 timu yake ilichopo...
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amelaumu makosa ya yaliyofanywa na mwamuzi Michael Oliver kwa kipigo cha 3-1 timu yake ilichopokea kutoka kwa Watford Jumapili.
Mashetani Wekundu waliangukia pua kipigo cha tatu mfululizo katika michuano yote baada ya Etienne Capoue, Juan Zuniga na Troy Deeney kutikisa nyavi kila mmoja katika uwanja wa Vicarage Road.

Mourinho, ambaye alidai kuwa utendaji duni wa mwamuzi ni moja ya sababu ya Manchester United kufungwa 2-1 dhidi mahasimu wao Manchester City, na ameuponda uwezo wa mwamuzi wa mechi dhidi ya Watford akiamini kuwa goli la Capoue halikustahili kuhesabiwa kwa sababu ya Miguel Britos kumchezea rafu Anthony Martial kabla ya goli hilo kupatikana.
"Naweza kuzungumzia mambo matatu - moja ni makosa ya mwamuzi, haimo ndani ya uwezo wangu," aliwaambia waandishi. "Siwezi kufanya lolote. Siwezi kabisa kubadili hilo.
"Lakini dhidi ya Man City mnajua kilichotokea dakika ya 55. Leo mmeona kilichotokea kwenye goli la kwanza, tumeadhibiwa kwa makosa haya waamuzi lakini siwezi kufanya chochote.
United watakuwa wakipambana kuepuka kipigo cha nne mfululizo wanapojiandaa kwenda Northampton kwa Kombe la EFL wiki hii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top