Unknown Unknown Author
Title: Tambwe na Ngoma wamkata Julio kidomo-domo
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom Yanga leo imeeneleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Mwadui FC, mabao 2-0, katika mchezo uliopigw...
Mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom Yanga leo imeeneleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Mwadui FC, mabao 2-0, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Yanga iliyotua Shinyanga kwa matatizo makubwa ya usafiri  huo ni mchezo wake wan ne kwenye ligi ya msimu huu ambapo imeweza kucheza bila kuruhusu bao kweye nyavu zake.
Mshambuliaji wa kimataifa raia ws Burundi Amissi Tambwe, ndiye aliyeanza kuiweka mbele timu yake ya Yanga kwa bao safi alilolifunga dakika ya tano kufuatia krosi nzuri ya Simon Msuva.
Mwadui inayofundishwa na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Jilio’ walijitahidi kupambana kwa kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini nahodha Nadir Haroub Cannavaro na Kelvin Yondani walifanya kazi yao vizuri kwa kuokoa mashambulizi yote.
Yanga ilijikuta ikipata pigo katika dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza baada ya kiungo Thabani Kamusoko kuumia ugoko na nafasi yake ilichukuliwa na Haruna Niyonzima.
Mchezo huo uliendelea kuwa wa kasi na kushambuliana kwa kila upande lakini hadi mapumziko matokeo yalibaki kuwa Yanga 1-0 Mwadui.
Kipindi cha pili Mwadui walikianza kwa kasi na kutafuta bao la kusawazisha lakini wachezaji wa Yanga walikuwa makini kuokoa mashambulizi yote.
Yanga ambao walicheza kwa kujiamini na kama wanavyokuwa uwanja wa taifa walipanga vizuri mashambulizi yao na kuliandama mara kwa mara lango la Mwadui lakini mara kadhaa Msuva na Niyonzima walishindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
Wakati mashabiki wa mchezo huo wakiamini Yanga itashinda bao moja mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma alifunga bao  la pili dakika ya 90 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Niyonzima na hilo kuwa bao lake la kwanza msimu huu.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo kwa kufikisha pointi 10 sawa na Azam lakini yenyewe haijaruhusu bao kwenye nyavu zake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top