toniking toniking Author
Title: Serengeti yaivutia kasi Congo
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
. TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys inaondoka leo kuelekea Rwanda kwa ajili ya kambi ya siku...


.
TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys inaondoka leo kuelekea Rwanda kwa ajili ya kambi ya siku 10
Serengeti inajiandaa na mechi ya marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wa umri huo dhidi ya Congo Brazzaville inayotarajiwa kuchezwa wiki ijayo.
Katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita, Serengeti iliiadhibu Congo kwa mabao 3-2 kupitia kwa Yohana Mkomola aliyefunga magoli mawili kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa na Issa Makamba kipindi cha pili.
Serengeti ilipata pigo kipindi cha pili baada ya kipa namba moja Ramadhani Kabwili aliyepata majeraha wakati akijaribu kuokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Langa-Lesse Percy.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kuwa wachezaji wana ari na kwamba mlinda mlango Kabwili anaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa timu hiyo aliokosa mechi ya kwanza wamerejea kikosini na watacheza mechi ya marudiano.

“Tunaamini Serengeti itafanya vizuri, wachezaji wana ari kubwa na wapo vizuri kisaikolojia, Ally Ng’azi na Dickson Job walikuwa na kadi za njano walilazimika kukosa mchezo wa Congo Brazaville taifa wakitumikia adhabu ya kadi lakini sasa mechi ya marudiano watacheza,” alisema Lucas.
Ng’azi alipewa kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Afrika Kusini uliofanyika Agosti 21, mwaka huu wakati Dickson alipewa kadi katika mchezo wa Shelisheli wa nyumbani alipewa kadi moja na marudio akapewa kadi nyingine na katika mchezo na Afrika Kusini alipewa pia kadi ya njano hivyo kufikisha idadi ya kadi tatu za njano na kulazimika kukosa mchezo mmoja.
Katika mchezo wa marudiano dhidi ya Congo utakaofanyika Oktoba 3 Serengeti inatakiwa kucheza kufa au kupona isiruhusu kufungwa ama ishinde ili ikate tiketi ya kucheza fainali hizo mwakani Madagascar

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top