toniking toniking Author
Title: Watengeneza makaburi hewa walipwe fidia
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wananchi mkoani Simiyu ambao maeneo yao yanapitiwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kw...
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wananchi mkoani Simiyu ambao maeneo yao yanapitiwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami wanadaiwa kutengeneza makaburi hewa tisa ili walipwe fidia na tayari wamelipwa sehemu ya fidia.
Imeelezwa kuwa Sh milioni sita zilitengwa kwa ajili ya kuwalipa fidia wenye makaburi hayo yaliyopitiwa na barabara na wananchi wengi walibainika kujenga makaburi hewa na kudai barabara imeyafuata.
Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Simiyu, Albert Kent, aliyasema hayo wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara mkoani hapa kilichofanyika mjini Bariadi.
Alisema makaburi manne yaligundulika kuwa hewa katika mradi ambao umemalizika ujenzi wake wa Lamadi-Bariadi, ambapo kaburi moja tu lilikuwa halali kati ya matano na katika mradi mpya wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi unaojengwa kwa kiwango cha lami, makaburi matano kati ya sita yalikuwa hewa.
Alisema katika makaburi hayo tayari wamiliki walikuwa wamelipwa fidia, ambapo walipata taarifa kutoka kwa raia wema na kuelezwa kuwa baadhi ya makaburi ni hewa.
Alisema katika makaburi hayo kiasi cha Sh milioni sita zilitengwa kulipia fidia, lakini baada ya kuchunguza Tanroads ililipa Sh 500,000 tu na pesa zilizobaki kurejeshwa serikalini.
Aidha, alisema katika kuhakiki makaburi hayo walikuwa wakiambatana na viongozi wa vijiji, ambapo wamiliki walikuwa wakiamriwa kufukua wao wenyewe kabla ya kulipwa pesa zao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top