Unknown Unknown Author
Title: Zeben Hernandez bado ana imani ya ubingwa Azam FC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Muhispania huyo amekiri kwamba wapinzani wao Ndanda walicheza vizuri zaidi yao lakini uwanja ulichangia pia wao kupoteza mchezo Baada...
Muhispania huyo amekiri kwamba wapinzani wao Ndanda walicheza vizuri zaidi yao lakini uwanja ulichangia pia wao kupoteza mchezo
Baada ya kipigo cha mabao 2-1, kutoka kwa Ndanda FC, kocha Mhispania wa Azam FC, Zeben Hernandez, amesema bado ana matarajio ya ubingwa msimu huu licha ya kupepesuka kwa mechi mbili zilizopita.
Hernandez ameiambia Goal,  ushindani umekuwa kubwa hasa wanapocheza ugenini lakini ameifurahia hali hiyo na kuwataka wachezaji wake kuongeza bidii ili kuhakikisha wanashinda mechi zijazo mbele yao.
“Wapinzani wetu walikuwa bora sana zaidi yetu nafikiri na uwanja ulipelekea sisi kupoteza mchezo huu kwasababu hatukucheza kwenye kiwango chetu na safu yangu ya ulinzi ilifanya makosa mengi lakini siwezi kumlaumu mtu ndiyo mambo ya mpira yanavyokuwa,” amesema Hernandez.
Azam imebakiwa na pointi zao 10 katika nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza michezo sita Simba ipo kileleni ikiwa na pointi 16, na mabingwa watetezi Yanga wanashika nafasi ya pili kabla ya mchezo wa leo wakiwa na pointi 10 huku wakiwa nyuma kwa michezo miwili dhidi ya Simba na Azam.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top