Goal inakuletea kikosi bora cha wiki baada ya michezo takribani 7 kupigwa Jumamosi na Jumapili
1.Frank Mwamongo
Mlinda mlango wa Stand United alikuwa kwenye ubora wa hali ya juu kuwazuia washambuliaji wa Yanga, aliweza kuwapanga mabeki wake vizuri na kuzuia mipira yote ya hatari langoni mwake anapata 1.
2.Hemed Khoja
Aliunda safu ngumu ya ulinzi dhidi ya Wana lamba lamba na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa Azam siku ya Jumamosi mjini Songea anapata 2.
3.Mohamed Hussein
Ameendeleza ubora wake alioanza nao msimu huu, alifanikiwa kupandisha timu mbele pindi wakiitaji kushambulia na kupiga krosi hatari langoni mwa Majimaji anapata 3.
4.Erick Mulilo
Ndiye kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kutopata goli dhidi ya Stand United, kisiki huyo alifanya kazi kubwa kuwadhibiti washambuliaji hatari wa Wana Jangwani aliondoa hatari zote langoni kwake hasa mipira ya juu anapata 4.
5.Method Mwanjali
Licha ya Majimaji kujaribu kutafuta goli Jumamosi dhidi ya Simba ila walikutana na kikwazo kutoka kwa Mzimbabwe Mwanjali, beki huyo mkongwe amefanikiwa kulinda timu yake kutoruhusu goli kwenye mechi 3 mfululizo anapata 5.
6.Jonas Mkude
Alitawala eneo la katikati dhidi ya Majimaji na kuwapa wakati mgumu viungo wa Wana Songea, na alifanikiwa kutengeneza goli la nne lilofungwa na Kichuya anapata 6.
7.Shiza Kichuya
Alifunga magoli kwenye ushindi wa magoli 4 kwa bila dhidi ya Wana lisombe, aliwapa wakati mgumu safu ya ulinzi wa Majimaji kwa uwezo wake wa kumiliki mpira na chenga za mahudhi anapata 7.
8.Pastory Anthony
Alipeleka msiba kwenye mitaa ya Jangwani kwa goli lake pekee dhidi ya mabingwa watetezi Yanga, kiungo mshambuliaji huyo wa Stand United ameipeleka klabu yake hadi nafasi ya 2 nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama 4 anapata 8.
9.Atupele Green
Ushindi wa JKT Ruvu kwa Mbeya City ulitokana na  nguvu kubwa,  kiwango bora cha green siku hiyo, mshambuliaji huyo alifunga goli moja na kutengeneza nafasi nyingi kwa wenzake licha ya kutotumiwa vizuri anapata 9.
10.Kelvin Sabato
Kwa mara ya kwanza safu ya ulinzi ya Yanga walikutana na wakati mgumu na mshambuliaji wa Stand United Kelvin Sabato, alifanikiwa kuyumbisha safu hiyo chini ya Vincent Andrew anapata 10.
11.Jamal Mnyate
Magoli mawili siku ya Jumamosi na Majimaji kwenye ushindi wa goli nne kwa bila, winga huyo alikuwa msumbufu kwa dakika zote za mchezo anapata 11.