Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm ameandika barua ya kujiuzulu kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani
“Nimeandika barua ya kujiuzulu kutokana na jinsi mambo yanavyokwenda, sikufurahishwa nayo. Nimeamua kujiuzulu na tayari nimekabidhi barua kwa uongozi wa Yanga, kama watapitisha nahitaji wanikamilishie stahiki zangu,” Van der Pluijm amenukuliwa akiongea kwenye simu kupitia Radio One.
Wakati huohuo, mzambia George Lwandamina amesema hajasaini mkataba wowote na Yanga ingawa amekiri Yanga inamuhitaji.
Amesema kwamba, kama watakubaliana yupo tayari kuja na kuipa Yanga mafanikio zaidi.
Post a Comment