Nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema inasikitisha kocha waliyemzoea kuondoka lakini wapo tayari kufanya kazi na kocha mpya
Cannavaro ameiambia Goal, kwamba wachezaji wameumizwa na jambo hilo lakini hawana namna ila wapo tayari kufanya kazi na kocha yeyote atakaye pendekezwa na uongozi wao kwakua ndiyo maamuzi yaliyofikiwa.
"Tumesikia kocha Pluijm amejiuzulu inaumiza kwa sababu wachezaji tulikuwa tumemzoea lakini hamna namna ispokuwa kama wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu na tupo tayari kumpa ushirikiano kocha mpya ajaye.
Cannavaro amesema wamejiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yoyote yale pasipo kuathiri mwenendo wa timu katika ligi na wanatambua thamani ya ubingwa wanao utetea kwa wanajangwani hivyo ni lazima kupambana ili kuutetea tena kwa mara ya tatu msimu huu.
Nahodha huyo ambae amedumu Yanga kwa miaka 10 amewaomba mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendeleza umoja na mshikamano waliokuwa nao hivi sasa ili waweze kutimiza kile wanachokikusudia.
Post a Comment