toniking toniking Author
Title: Maofisa TFF wamefikishwa mahakamani leo Nov 9 2016
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya headlines za muda mrefu na tuhuma za baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka  Tanzania TFF  kudaiwa kuomba rushwa ili wawez...



Baada ya headlines za muda mrefu na tuhuma za baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF kudaiwa kuomba rushwa ili waweze kupanga matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza ili wa wapande Ligi Kuu.
Leo November 9 2016 Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURUwamekamilisha uchunguzi wao na kuwafikisha mahakamani maofisa wawili wa TFF Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi na  Martine Chacha.

Martine Chacha

Matandika na Chacha wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh milioni 25 kutoka timu ya Geita Gold ili waisaidie kupanda  Ligi Kuu kutoka Ligi daraja la kwanza.
                                                         
Kwa pamoja Matandika na Chacha wamekana mashtaka na wapo nje kwa dhamana ya Tsh milioni 5 kila mmoja na kesi yao imeahirishwa hadi November 30, wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo February 4 2016 katika ofisi za TFF.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top