toniking toniking Author
Title: Bwana harusi akataliwa kuoa siku ya harusi
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
Heka Heka ya Leo November 9 2016 kwenye leo Tena ya Clouds FM ni kuhusu Bwana harusi aliyekataliwa kuoa dakika za mwisho za harusi huku ...

Heka Heka ya Leo November 9 2016 kwenye leo Tena ya Clouds FM ni kuhusu Bwana harusi aliyekataliwa kuoa dakika za mwisho za harusi huku taratibu zote zikiwa zimefatwa kwa kutolewa barua na mahari huku bibi harusi akiwa ameshafanyiwa kitchen party na mama yake.
Imeelezwa kuwa sababu iliyopelekea bwana harusi kukataliwa ni kutokana na baba mzazi wa bi harusi kutokushirikishwa kwenye chochote na mama wa bi harusi mpaka siku hiyo ya ndoa alipopewa taarifa na akaamua ndoa isifungwe.
>>>”Nilipanga mwanangu aolewe lakini baba mtu nikawa sijamshirikisha niliwaambia  ndugu zangu baba mtu kakataa kasema haolewi ndio basi, tumetengana siku nyingi mimi na baba yake na barua ilivyopelekwa hatukumpelekea, mtoto nimemlea mwenyewe lakini huwa anaenda tu kwa baba yake kumsalimia” – Mama wa Bibi Harusi
>>>”Baba kapigiwa simu akasema mtoto asiolewe basi tukakubali ndoa ivunjwe, mimi sijui wanajuana wenyewe wazazi, ndio tushamalizana tena zawadi zangu nimepewa kama mwali wa kawaida  sio bi harusi tena”- Bibi Harusi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top