Unknown Unknown Author
Title: Samaki anayejiponya uti wa mgongo
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watafiti nchini Marekani wamesema wamebaini aina fulani ya samaki anayeweza kuzalisha upya uti wake wa mgongo unapovunjika wanaweza kus...
Watafiti nchini Marekani wamesema wamebaini aina fulani ya samaki anayeweza kuzalisha upya uti wake wa mgongo unapovunjika wanaweza kusaidia kubuni matibabu yatakayoweza kuwasaidia watu waliopooza kutembea tena.
Wanasayansi wamegundua kuwa samaki huyo ajulikanaye kama Zebra Fish anapovunjika uti wa mgongo, huzalisha sehemu nyingine ya uti wa mgongo na kuunganisha kama daraja sehemu zilizokatika kwa kutumia aina ya protini mwilini mwake.
Wanadamu wanayo aina hiyo ya protini inayoweza kuzalisha mifupa lakini haifanyi kazi sawa na ile ya samaki huyo.
Aina hiyo ya protini kwenye binadamu inafanana kwa asilimia 90 na aina hiyo kwenye samaki hao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top