Unknown Unknown Author
Title: unior Kabananga aongoza mbio za kiatu cha dhahabu AFCON 2017
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nyota wa Congo DR Junior Kabananga ndiye kinara wa mabao AFCON 2017 hadi sasa akiwa ametupia goli moja kila mechi na kufikisha jumla ya m...
Nyota wa Congo DR Junior Kabananga ndiye kinara wa mabao AFCON 2017 hadi sasa akiwa ametupia goli moja kila mechi na kufikisha jumla ya mabao matatu
DR Congo wametinga hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika wakiwa wanaongoza Kundi C kwa ushindi uliowatupa nje ya michuano Togo.
Mchezaji anaeongoza kwa kufumania nyavu kwenye mashindano hayo hadi sasa Junior Kabananga alifunga bao la kwanza kwa timu yake huku likiwa ni goli lake la tatu kwenye mechi ya tatu.
Kabananga alipiga kichwa na mpira kugonga post kabla ya Ndombe Mubele kuiandikia DR Congo bao la pili dakika chache baada ya mapumziko.
Kodjo Fo-Doh Laba aliifungia Togo bao na kuipa matumaini lakini goli la Paul-Jose M’Poku lililotokana na mkwaju wa free-kick likaihakikishia DR Congo ushindi.
DR Congo inatarajia kucheza na mshindi wa pili wa Kundi D kwenye mchezo wa robo fainali ambapo Mali, Ghana au Misri ndio timu zenye nafasi ya kukutana na watoto wa Kabila.
Togo walihitaji ushindi pekee dhidi ya DR Congo ili wasonge mbele kwenye hatua ya robo fainali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top