Unknown Unknown Author
Title: Ronaldo amemtaka Philippe Coutinho kutua Real Madrid
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ronaldo amesema soka la Hispania, bila shaka ni bora zaidi katika historia na itakuwa ni vema kwa Coutinho kuthubutu kucheza na wachezaji...
Ronaldo amesema soka la Hispania, bila shaka ni bora zaidi katika historia na itakuwa ni vema kwa Coutinho kuthubutu kucheza na wachezaji bora duniani
Mshindi wa Kombe la Dunia Ronaldo amekiri kuwa angependa kumuona kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho akicheza Real Madrid.
Nyota huyo, 24, amekuwa akifanya vizuri tangu alipotua Anfield akitokea Inter Milan mnamo 2013, tetesi zikipamba moto kuwa Barcelona au Paris Saint-Germain zinaitaka huduma yake.
Hata hivyo, Ronaldo anataka kumwona Mbrazili mwenzake Coutinho - ambaye ana mkataba Liverpool hadi 2020 - akihama meli na kujaribu maisha mengine na wachezaji bora wa La Liga wanaokipiga Real Madrid.
"Ningependa kumwona Coutinho Real Madrid," aliiambia redio ya Hispania Onda Cero. "Soka la Hispania, bila shaka, ni bora katika historia. Wamekuwa wakinunua wachezaji bora na kuzalisha soka lenye mvuto zaidi."
Ronaldo amecheza miaka mitano Bernabeu, akifunga mara 104 katika mechi 177 Real Madrid na kuiwezesha timu yake kutwaa mataji mawili Hispani

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top