Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC kutwaa tuzo hiyo
Alfred Lucas amemtangaza Kichuya kushinda tuzo hiyo akifuata nyayo za John Boco aliyeshinda tuzo hiyo kwa mwezi Agosti.
Kichuya amewashinda washambuliaji Adam Kingwande wa Stand United na Omary Mponda wa Ndanda FC.
Kichuya aliisaidia klabu yake ya Simba katika mwezi Septemba kupata pointi 12 katika mechi nne ambazo ilicheza, matokeo ambayo yameifanya Simba kuendelea kuongoza ligi.
Alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne alizocheza. kwa kushinda tuzo hiyo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa mdhammini wa ligi kuu Tanzania bara.
Post a Comment