Klabu nyingi za Ligi Kuu zimezalisha magoli mengi kupitia viungo wao wa pembeni kuliko hata washambuliaji asilia
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa takribani mwezi mmoja na itarejea tena Disemba 17 kwa ajili ya mzunguko wa pili Mnyama Simba bado yupo kileleni kwa tofauti ya alama mbili mbele ya klabu ya Yanga
Duru la kwanza Ligi Kuu Bara unaweza sema lilikuwa na neema kwa viungo wengi wanao cheza pembeni kwani wengi wao wamekuwa bora mzunguko wa kwanza kwa kuweza kufamania nyavu zaidi ya washambuliaji wa kati , mawinga hao wa karibu kila timu ndiyo wamekuwa wakitumika kuleta matokeo chanya kwenye timu zao iwe kwa kufunga wao au kusaidia kwa wengine
Goal inakuletea mawinga bora Ligi Kuu kwa mzunguko wa kwanza Tanzania bara
Amekuwa bora chini ya mwalimu Mcameroon Joseph Omog na ndiye mchezaji bora kwa duru la kwanza, kiungo huyu wa zamani Mtibwa Sugar amekuwa na mchango wa moja kwa moja kwenye klabu yake ya Msimbazi kwenye michezo 15 ya awali Ligi Kuu kwani ameweza kufunga magoli 9 na kusaidia matano kwa wenzake
Winga wa klabu ya Yanga ameendeleza makali yake ya miaka yote, Simon Msuva amefunga magoli 7 na kutengeneza magoli 13 kwa wenzake kwenye mechi 15 za mzunguko wa kwanza pekee pia faida yake kubwa uwanjani ni kasi yake na ndiyo imekuwa kikwazo kwa mabeki wengi kushindwa kumzuia
Tayari amefunga magoli 5 mpaka sasa Chanongo anayekipiga Mtibwa msimu huu akitokea Stand United, amekuwa akitumika kama silaha ya mashambulizi yote ya Wakata miwa pindi wakishambulia pia amekuwa akitoa msaada mkubwa kwa washambuliaji wa kati kwa kutengeneza nafasi nyingi kwao
Siyo jina kubwa hapa nchini ila kinda huyu amekuwa na kiwango cha kushangaza duru la kwanza uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kutengeneza nafasi hali kadhalika kufumania nyavu maana kwani mpaka sasa amefunga magoli 4 kwenye mechi 15
Post a Comment