Unknown Unknown Author
Title: Mwindaji aliyeua Simba aondolewa mashtaka Zimbabwe
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mahakama nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi dhdi ya muwindaji Theo Bronkhurst, inayohusu mauaji ya simba kwa Jina Cecil aliyeuawa mwak...
Mahakama nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi dhdi ya muwindaji Theo Bronkhurst, inayohusu mauaji ya simba kwa Jina Cecil aliyeuawa mwaka 2015.
Simba huyo aliuawa na daktari raia wa Marekani mwezi Julai mwaka 2015, kisa ambacho kilishutumiwa kote dunaini.


Simba huyo wa umri wa miaka 13 amekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kwenye mbuga ya kitaifa ya Hwange nchini Zimbabwe.Zimbabwe ilimlaumu Theo Bronkhurst kwa kumhadaa Cecil kutoka nje ya mbuga hiyo, na kisha kuuawa na mwindaji akitumia mshale.
Cecil alikuwa amewekewa kifaa cha kumfuatilia cha GPS kwa utafiti na chuo cha Uingereza cha Oxford.
Mauaji ya Cecil yalisababisha kuanza kwa kampeni ya kimataifa ya kumaliza uwindaji wa Simba

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top